Federico Valverde kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Uruguay, ametangazwa rasmi kua mchezaji bora wa mwezi wa tisa ndani ya klabu hiyo.

Kiungo huyo amekua na kiwango bora sana ndani ya mwezi tisa ndani ya klabu hiyo kitu kilichomfanya kufanikiwa kua mchezaji bora wa mwezi ndani ya klabu hiyo.

fede valverdeFederico Valverde amekua mchezaji muhimu kwenye kikosi cha mwalimu Carlo Anchelotti, Uwezo wa kiungo kupanda toka mwanzoni mwa msimu uliomalizika lakini kiwango chake kinaonekana kuimarika kila siku na msimu ameongeza kitu kikubwa kwenye mchezo wake.

Valverde ameongeza uwezo hasa kwenye upande wa kufunga magoli kwani msimu huu tayari ameshafunga magoli kadhaa hasa katika mwezi huu ambao amepewa mchezaji bora wa mwezi baada ya kufunga magoli katika michezo mitatu ya mwisho ya klabu hiyo kati ya Real Mallorca,Rb Leipzif, pamoja Athletico Madrid. Pia amefanikiwa kupiga pasi za mbili za mabao katika michezo miwili kati ya Real Betis katika ligi kuu na Celtic katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya.

federico valverdeTuzo hii kwenda kwa kiungo huyo ndani ya mwezi watu mashabiki wengi hawajatia shaka kutokana na uwezoaliounesha ndani ya mwezi huo baada ya kuhusika kwenye magoli matano kitu ambacho hakijafanywa na mchezaji yeyote ndani ya klabu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa