KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum amefunguka kuwa licha ya kuwa na rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi mpaka sasa lakini mipango yao ni kuweka rekodi hiyo mpaka kumalizika kwa msimu huu.

Yanga mpaka sasa tayari wamecheza mechi 44 za ligi kuu bila kupoteza ambapo kwa msimu huu tayari wamekusanya pointi 17.

Kikosi cha Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi jana jumatano kilifanikiwa kuendeleza rekodi hiyo baada ya kuibuka na ushindi mbele ya KMC kwa bao 1-0.

Feisal alisema kuwa katika mchezo huo wa jana licha ya kufunga bao la ushindi lakini hali yake ya afya haikuwa nzuri kutokana na tumbo kumsumbua.

“Kwanza namshukuru Mungu kwa kuisaidia timu yangu kupata ushindi kwenye mchezo wa leo kwani pointi tatu zilikuwa muhimu.

“Nilikuwa nianze kwenye mchezo wa leo lakini tumbo lilikuwa linanisumbua hivyo nilipoingia nilifuata maelekezo ya kocha ndio maana tumeibuka na ushindi.

“Rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi ni mwendelezo hivyo sisi tunajipanga kama wachezaji kuitetea nembo ya klabu tusipoteze mechi hata moja mpaka kufikia mwishoni mwa msimu huu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa