Manchester United wameibuka na ushindi wa 5-2 dhidi ya Ipswich Town, huku Bruno Fernandes akiwa shujaa wa mchezo baada ya kufunga hat-trick. Ipswich walianza kwa nguvu na kuongoza kupitia Leif Davis, lakini United waligeuza mchezo haraka.

Marcelino Nunez alipoteleza, Matheus Cunha akamtengenezea Fernandes nafasi ya kusawazisha. Jacob Greaves akajifunga mwenyewe baada ya shuti la Harry Maguire, kabla Fernandes kuongeza la tatu kwa mkwaju wa penalti baada ya Cunha kuangushwa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Bruno hakusimama hapo. Alikamilisha hat-trick baada ya mashuti ya Kobbie Mainoo na Bryan Mbeumo kuzuiwa, kisha akamtengenezea Mbeumo nafasi ya bao la tano kupitia pasi ndefu iliyovunja ulinzi wa Ipswich.
Hat-trick hiyo imefikisha Fernandes kwenye mabao 113 katika michezo 330 akiwa na United. Pia imekuja siku chache baada ya kutangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA, kufuatia msimu uliopita ambapo aliweka rekodi ya Premier League kwa assists 21.

United walimaliza mchezo wakiwa wamepiga mashuti 33, idadi yao kubwa zaidi kwenye Premier League tangu 2016. Ipswich walipata bao la kupunguza maumivu kupitia mchezaji Chuba Akpom, lakini usiku ulikuwa wa nahodha aliyeiongoza United kutoka nyuma hadi ushindi mkubwa wa 5-2.


