Fernando Carlos Redondo Neri wengi wanamfahamu kama Fernando Redondo mzaliwa wa Argentine katika jiji la Benouis Areas mnamo mwaka tarehe 6 mwezi wa sita 1969.

Kiungo huyo fundi alivitumikia vilabu vya Argentine Juniors,Telleres vyote vya nchini kwao kabla ya kwenda nchini Hispania kujiunga na Tennerife kabla ya kujiunga na Miamba ya nchini Real Madrid.

Ubora wa kiungo huyo fundi wa mpira ulianza kuonekana baada ya kutua katika klabu ya Real Madrid mwaka 1994 na kuonesha ubora mkubwa mpaka kufikia kuitwa El Principle kwa maana ya mfalme kutokana na ubora aliounesha klabuni hapo.

fernando redondoRedondo alifahamika kama kiungo wa ulinzi mwenye uwezo mkubwa pia katika kuanzisha mashambulizi pale anapohitajika kufanya hivo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira,kupiga pasi,pamoja na ufundi mwingi aliokua nao mguuni mwake.

Kiungo huyo amecheza kwa mafanikio makubwa ndani ya Madrid na kufanikiwa kubeba mataji kadhaa ikiwemo mataji mawili ya La liga pamoja na mataji mawili ya ligi ya mabingwa ulaya mwaka 1998, na mwaka 2000 ambao ndio ulikua msimu wake wa mwisho kuwatumikia Galacticos.

Kiungo huyo anakumbukwa zaidi kwa ufundi wake klabuni hapo zaidi ubora aliouonesha katika mechi ya robo fainali mwaka 2000 ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Manchester united katika dimba la Old Trafford na kuchaguliwa kua mchezaji bora wa michuano mwaka huo.

Kiungo huyo aliondoka Madrid mwaka 2000 na kuelekea klabu ya Ac Milan ambapo alidumu kwa miaka minne tu huku akicheza michezo michache huku akifanikiwa kushinda taji la ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2003 pamoja Coppa Italia.

fernando redondoFernando kwenye ngazi ya kimataifa pia ameitumikia timu yake ya taifa ambapo anakumbukwa zaidi kwa mkasa wake wa kukataa kushiriki kombe la dunia mwaka 1990 baada ya kuitwa huku mwanzo akidai alikua anasomea masomo yake ya sheria lakini baada alikuja kufunguka hakua anavutiwa na mbinu za kocha wakati huo Carlos Salvador Bilardo na kusema alijua ataitwa ila hataenda kuanza ni bora kubaki nyumbani.

Redondo alishiriki kombe la dunia na timu ya taifa ya Argentina mwaka 1994 mwaka 1998 kombe la dunia lililochezwa nchini Marekani kiungo huyo aligomea tena timu ya taifa iliokua chini ya mwalimu Daniel Passarella huku yeye akidai kocha huyo alikua ana sheria kali za kinidhamu akimtaka anyoe nyele zake na yeye akagoma kutii amri hiyo.

Redondo amefanikiwa na Argentina baada ya kubeba kombe la King fahd mwaka 1992 pamoja na Copa America mwaka 1993.

Kiungo huyo fundi pia ana mafanikio yake binafsi kama mchezaji bora wa ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2000,kuingia kwenye kikosi bora cha dunia mwaka 1996,mchezaji bora wa mwaka wa klabu ya Real Madrid mwaka 1997,1999, na mwaka 2000.

Fernando Redondo alistaafu soka rasmi mwaka 2004 akiwa katika klabu ya Ac Milan huku akisumbuliwa sana na majeraha mwisho wa kipindi chake cha kucheza mpira.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa