Kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Fernando Santos amesema kikosi chake hakikabiliwi na presha ya aina yeyote kuelekea mtanange dhidi ya majirani zao timu ya taifa ya Hispania utakaopigwa usiku wa leo.

Ureno wakiwa wanaongoza kundi wakiwa na alama zao 10 huku wakifuatiwa na Hispania ambao watamenyana katika mchezo huo wa mwisho ambao utaamua ni nani ataweza kufuzu katika nusu fainali za michuano ya Uefa Nations League.

fernando santosSantos anasisitiza vijana wake hao hawana presha kuelekea mchezo huo usiku wa zaidi ya hali hewa iliyopo wakati huu kikosini hapo,Mchezo huo ambao unazikutanisha timu hizi Ureno wanahitaji suluhu tu katika mchezo huo ili kufuzu hatua inayofuata ya nusu fainali huku Hispania wao wakihutaji ushindi.

 

Hichi kinaweza kua kipimo kizuri kwa mwalimu Santos timu yake kuelekea michuano ya kombe la dunia nchini Qatar baadae mwaka huu  ambapo timu hiyo inaonekana kua na wachezaji wengi wazuri lakini imekua ikipata matokeo ya kwa kusuakusua.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa