Fifa Awards: Lewandowski, Chelsea Wameng'ara!

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Robert Lewandowski ameondoka na tuzo kubwa ya dunia, Fifa Awards zimetaradadi.

Januari 17,2022 bila shaka itabaki kuwa siku ya historia kwenye maisha ya Lewandowski na klabu ya Chelsea kwa ujumla wake.

Baada ya figisu za kukosa tuzo ya Ballon d’Or kwa misimu miwili mfululizo – 2020 tuzo haikutolewa, 2021 alipewa Lionel Messi, Lewandowski ameibuka kidedea kwenye tuzo kubwa za dunia – Fifa Awards. Hizi ni tuzo ambazo hutolewa kwa wachezaji, makocha na timu zilizofanya vizuri duniani kwa mwaka husika.

Kikosi Bora cha Mwaka. Chanzo: BBC

Bila shaka, takwimu na ubora wa Lewandowski unajidhihirisha wazi kuwa, anastahili heshima ambayo imekua ikimkwepa kila mara. Utalawa wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ni kama haupo tena. Lewandowski, Benzema, Salah na Haaland ni washambuliaji hatari duniani kwa sasa.

Katika kudhihirisha ubora na heshima anayostahili, Robert Lewandowski ametunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Fifa (wanaume) huku timu ya Chelsea ikitoa Kocha bora (wanaume na wanawake), wachezaji 2 (viungo) wapo kwenye kikosi bora cha mwaka pamoja na tuzo ya golikipa bora wa mwaka.

Orodha ya washindi wa Fifa Awards:

Mchezaji Bora wa Mwaka (Wanaume): Robert Lewandowski

Kocha Bora wa Mwaka (Wanaume): Thomas Tuchel

Golikipa Bora wa Mwaka (Wanaume): Edouard Mendy

Tuzo Maalumu ya Fifa: Cristiano Ronaldo

Goli Bora la Mwaka: Erik Lamela

Tuzo ya Mashabiki wa Mwaka: Denmark & Finland fans

Tuzo ya Uungwana: Denmark national team/Danish medical team and coaching staff

Mchezaji Bora wa Mwaka (Wanawake): Alexia Putellas

Kocha wa Mwaka (Wanawake): Emma Hayes

Golikipa wa Mwaka (Wanawake): Christiane Endler

Tuzo Maalumu ya Fifa: Christine Sinclair


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe