FIFA kufanya kikao kwa njia ya mtandao siku ya kesho tarehe 20 Disemba kujadili kuhusu kufanyika kwa michuano ya kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili, huu ni muendelezo wa vikao vya kushawishi nchi wanachama kuweza kupitisha azimio hilo.
Tokea kuibuliwa kwa wazo la kufanyika kwa mashindano hayo makubwa ya Dunia kwa ngazi ya timu za taifa, kumetokea upinzani mkubwa hasa bara la Ulaya ambapo wanadai kwanza ni kupoteza mvuto wa mashindano ikiwa yatakuwa yanachezwa kila baada ya miaka miwili, pili ni kuchosha wachezaji kutokana na mashindano kuwa mengi.
FIFA inapata nguvu ya kuweza kuisukuma ajenda yake hiyo kutokana na kukubalika kwa ajenda hiyo kwenye mabara yaliyo na wanachama wengi kama Afrika Asia na South America
Raisi wa FIFA Gianni Infantino alielezea faida ya michuano kufanyika kila baada ya miaka miwili ni kufungua njia timu ndogo kuweza kushiriki mara kwa mara kutokana na kuongeza idadi ya timu, pia itawasaidia FIFA kupata pesa zaidi za kuweza kusaidia mabara tegemezi kama Afrika na America.
Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.