Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeifungia klabu hiyo kusajili kwa kipindi kimoja kijacho cha usajili.
Hukumu hiyo ya FIFA imekuja kufuatia shirikisho hilo kuikuta na hatia Simba kutokana na kushindwa kumalizana na beki wao wa zamani, Mghana Asante Kwasi.
Taarifa kutoka nchini Ghana zinasema adhabu hiyo kwa Simba itaanza kufanya kazi katika dirisha lijalo la usajili.
Imeelezwa kuwa Simba ilipewa muda wa kukamilisha malipo ya mchezaji wao wa zamani, Asante Kwasi ambaye alipeleka malalamiko yake Shirikisho la Soka Duniani, (FIFA) ili kupata stahiki zake.
Kwa mujibu wa barua ambayo waliandikiwa Simba kutoka Shirikisho la Soka la mpira la Ghana, PFAG liliwaeleza kuwa wanapaswa kumlipa mchezaji huyo stahiki zake baada ya kushinda rufaa.
Barua hiyo iliandikwa Februari 26,2021 zama za Mtendaji Mkuu, Senzo Mbatha ambaye kwa sasa ni Mshauri wa kuelekea kwenye Mabadiliko ndani ya Yanga.
Maamuzi ya Fifa yalifanyika awali Januari 15,2020 na pia shauri la pili likatolewa maamuzi Februri 2021 baada ya mchezaji huyo kukata rufaa.
FIFA iliwaambia Simba kwamba wanapaswa kulipa kiasi cha USD 4,000 kwa ajili ya malipo ya stahiki za mchezaji Kwasi ambaye alicheza Simba akitokea Klabu ya Lipuli.
Habari zimeeleza kuwa Simba wamepewa muda kukamilisha malipo ya mchezaji huyo ambaye msimu wa 2017 alicheza Lipuli akitokea Klabu ya Mbao na aliachwa Simba msimu wa 2019
Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.
warda
Kweli penye riziki hapakosi fitina Simba inaelekea kwenye mafanikio ndo kesi kila siku zinaibuka ila watashinda tu
Johnmary jo
Ee jamani pole yao klabu ya simba ila yatakwisha na ushindi lazima#meridianbett#
Elika
Wanafanya vibaya
Adelta
Sawa tu ila simba iko kwenye mafanikio
aisha
Duuh sio powa kabisa
Magdalena
Wanahisi wanakomoa kumbe ndo kwanza wanazidi kuwafungulia milango ya baraka
Khadija
Majungu hayo
Sarah
Sio poa
Lydia Emmanuel Magoti
Duuh sio poa