Fletcher Kukaa Benchi 1 na Solskjaer.

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United – Darren Fletcher, amejiunga na benchi la ufundi la kikosi cha kwanza klabuni hapo.

Fletcher aliitumikia Man United kwa miaka 20 na alifanikiwa kutwaa mataji kadhaa ikiwemo EPL (5), FA (1), EFL (2), UEFA (1), FIFA Club World Cup (1) na aliichezea timu ya Taifa ya Scotland michezo 80.

Akiwa ni zao la mfumo ya akademia klabuni hapo, Darren Fletcher aliitumikia United kama mchezaji wa kikosi cha kwanza kwa jumla ya michezo 340 kuanzia mwaka 2003-2015.

Darren Fletcher alipokuwa mchezaji wa Man United.

Alikuwa akikinoa kikosi cha U16 cha United na sasa amepandishwa daraja na ataungana na Ole Gunnar Solskjaer kwenye kikosi cha kwanza.

Akizungumzia uteuzi huu, Solskjaer amesema “Darren anaDNA ya United kwenye mishipa yake ya damu na anajua nini kinahitajika ili uwe mchezaji wa Manchester United.

“Ndio anaianza safari yake ya ukocha lakini uzoefu wake ndani na nje ya uwanja pamoja na akili yake ya ushindi, kujitoa kikamilifu na ufanyaji kazi kwa bidii vitaongeza chachu kwenye kikosi chetu.”

Darren amenukuliwa akisema “Nimefurahi kurejea kwenye timu hii nikiwa kama kocha wa kikosi cha kwanza. Ni kikosi kizuri kinachovutia, ndio ninaianza safari yangu ya ukocha na nipo tayari kufanyakazi na Ole pamoja na wenzake”

Man United watakuwa uwanjani Jumatano hii kuwakabili Man City katika mchezo wa Nusu fainali ya Carabao Cup.


JIUNGE NA FAMILIA YA MERIDIANBET BURE!!!!

Ndio, kwetu Mteja ni mfalme. Jiunge sasa na familia ya Meridianbet bila malipo yeyote na sisi tutakuzawadia bonasi ya shilingi 3,500 kama sehemu ya kukukaribisha kwenye familia hii BURE!!!. Unasubiri nini??

BOFYA HAPA

14 Komentara

    Good New

    Jibu

    Iyo iko vizuri

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki

    Jibu

    Naona OLE anazidi kupewa silaha wanataka kuchukua ubingwa msimu huu

    Jibu

    iko poa

    Jibu

    Ole Yuko vizuri ushindi lazima

    Jibu

    Vizuri sana

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Good

    Jibu

    Inapendeza

    Jibu

    Wazee wa ot

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

    Inapendeza

    Jibu

Acha ujumbe