Wakati Real Madrid wakiingia kwenye kipindi cha mwisho cha msimu, mengi yamesemwa juu Eden Hazard zaidi ni mazungumzo kuhusu majeraha yake.

Florentino Perez Bado Ana Imani na Hazard

Baada ya upasuaji wake wa hivi karibuni, Hazard hatakuwa na jukumu muhimu katika Ligi ya Mabingwa au La Liga. Hilo litatawala vinywa vya mashabiki katika maisha yake yote ya Real Madrid.

Hata hivyo bado ana msaidizi mmoja muhimu sana ndani ya Real Madrid. Rais Florentino Perez hayuko tayari kuachana na Mbelgiji huyo bado.

Licha ya kuwa na misimu mitatu ya kutofanya vizuri, Florentino Perez bado ana imani na staa huyu. Sport wanasema Perez aliandamana na Hazard kwenye upasuaji wake kama ishara ya kumuunga mkono.

Jaribio la Real Madrid kumleta Kylian Mbappe na Erling Haaland lingepunguza sana nafasi yake ya kucheza. Ikiwa Haaland ataenda kwingine, anaweza kuwa na nafasi ya kutetea nafasi yake kwa msaada wa Florentino Perez. Zaidi ya hayo, Hazard mwenyewe anataka kufanikiwa akiwa  Real Madrid.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa