Foden Atimka Kambi ya Timu ya Taifa ya Uingereza

Kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester City Phil Foden ameripotiwa kuondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza na kurejea nyumbani.

Chama cha soka nchini Uingereza kimeeleza kua Foden amerejea nyumbani nchini Uingereza kutoka nchini Ujerumani ambapo michuano ya Euro  2024 inapigwa, Chanzo cha kuondoka kwenye kambi ya timu hiyo kimeelezwa ni kutokana na matatizo ya kifamilia ambayo yanamkabili.fodenMatatizo ya kifamilia ambayo yanamkabili kiungo mpaka sasa hayajawekwa wazi lakini taarifa ya chama cha soka nchini humo ndio kimeeleza taarifa hiyo, Mpaka wakati huu haijaelezwa kua atarejea lini kwenye kambi ya timu hiyo ambapo kwasasa wanasubiria kucheza hatua ya 16 bora.

Ikumbukwe mwaka 2022 kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar ilitokea kwa wachezaji wawili kwenye kikosi cha Uingereza kuondoka kambini na kurejea nyumbani ambao walikua ni Raheem Sterling, pamoja na Ben White kwajili ya kutatua matatizo ya kifamilia kama ilivyo kwa Phil Foden.

Acha ujumbe