Morocco Waanza Kwa Kishindo WAFCON 2026

Morocco wameonyesha ubabe wao mara moja kwenye TotalEnergies CAF Women’s Africa Cup of Nations 2026, wakishinda 4-0 dhidi ya Kenya katika mechi ya ufunguzi ya Kundi A mjini Rabat.

Morocco Waanza Kwa Kishindo WAFCON 2026

Magoli ya Ushindi yalifungwa Sakina Ouzraoui aliyefungua ukurasa kwa shuti la chini dakika ya 20. Meriem Atiq akaongeza kwa kichwa dakika ya 28. Ibtissam Jraidi akafunga mara mbili, dakika ya 40 na 47, akionyesha ubora wake kama mshambuliaji tegemeo wa Atlas Lionesses.

Hali ya Kundi A mpaka sasa ni Morocco waliopo kileleni kwa tofauti ya magoli, mbele ya Algeria waliowashinda Senegal 2-0. Senegal wanashika nafasi ya tatu. Kenya wako mkiani baada ya kurudi kwenye fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu 2016.

Morocco Waanza Kwa Kishindo WAFCON 2026

Baada ya mchezo huo, makocha walitoa kauli zao kuhusu mchezo huo ambapo kocha wa Kenya, Beldine Odemba alisema, “Hatukuwa na udhibiti wa kutosha kwenye transition ya mchezo. Tuna mechi mbili dhidi ya Senegal na Algeria, ni juu yetu kurekebisha makosa.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa upande mwingine, kocha wa Morocco Jorge Vilda alisema, “Ni mwanzo mzuri. Ukiyanza mashindano kwa namna hii, inamaanisha maandalizi yamekuwa mazuri.”

Morocco Waanza Kwa Kishindo WAFCON 2026

Mashindano haya ya timu 16 pia ni njia ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake 2027 nchini Brazil. Nusu fainali nne zitafuzu moja kwa moja, huku robo fainali mbili zikielekea kwenye mchujo wa inter-confederation.

Kwa Morocco, ushindi huu ni ujumbe wazi kwamba mara baada ya kumaliza kama washindi wa pili mara mbili mfululizo, sasa wanataka kutwaa taji kwa mara ya kwanza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.