Al Ahly hii au nyingine? Nilijiuliza lakini nikiri wazi nilianza kushtuka, nikaamini wazi CEO anatupanga, nikaona ameamua kutufunga kamba ila kuna sauti ikaniambia fanya research jiridhishe, usipinge tu.

Nikaanza kuwatafiti Ahly kisha nikawatafiti hata majirani zao Zamalek kisha nikaja kurelate na wale Pyramids, kuna kitu nikakigundua kwenye soka la Waarabu, hapo ndipo nikaanza kukubaliana na Barbara

al ahly
al ahly

Waarabu hawaamini sana kwenye sayansi ya soka, Waarabu pia ni conservative sana (hawabadiliki) na nikagundua Godfather wa soka lao ni Hassan Shehata, mnamkumbuka?

Shehata hakuwa Mwalimu wa kutisha sana ila ni Mastermind kwenye kuhamasisha, wana msemo wao unaitwa “eish aw mit” yani tufe au tuishi, soka lao linapigwa kwenye hamasa zaidi

Al Ahly
Al Ahly

Nikaja kugundua, hata tactically wana maeneo yao strategically ambayo wanacheza Waarabu tu, kwakuwa mbinu yao kubwa ni soka la kasi (Intesity) ndio maana ukiwanyima au ukiwazidi kasi tayari umewapoteza, wana mbinu moja tu

Waarabu wana driver mmoja katikati ambaye ni holder mzuri ila pembeni yake anakuwepo Mtu mwenye upepo, Ahly wana Aliou Dieng akishakaba mali inawekwa kwa El Soulia, timu yote inafunguka kwa kasi

Al Ahly


Zifuatilie timu zao zote, pembeni kunakotaka kasi kuna Waarabu tupu,Al Ahly wana Hany na Ashraf, juu wana Tahir Mohamed na Hussein El Shehat, wote waarabu na wote wana mwendo

Pitso Mosimane alijaribu kumleta Walter Bwalya akataka kuleta kitu kipya ila kilichomtokea ni kuwa Waarabu hawajui anachotaka, wakafeli ikabidi arudi kwenye utamaduni wao wa Mwendo, alitaka kuleta Watalaam wa Analyst wakagoma, wanaishi utamaduni wao

Simon Msuva kule Morocco ni mfano mwingine, alienda kama Winger ila mnaweza kuamini Waarabu wanamwona Msuva hana kasi? Wakamtoa pembeni na kumpeleka kati, kule wameweka Waarabu

Alichosema Barbara kuhusu Kiongozi wa Al Ahly ni kweli, Waarabu wana mbinu moja pekee, na mpira wao hauchambuliki mpaka kesho kinachowabeba ni Jihad, Ima tufe Ima tuishi, dunia imebadilika ila wao bado

Ilianza kwa Shehata na Misri, ikaenda Ahly kisha imesambaa Kaskazini kote


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA


ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa