Baada ya Martial, Nani Anafuata United?

Purukushani za Anthony Martial zimefanikisha usajili wake kwenda Sevilla, baada ya Martial, nani anafuata kuondoka Man United Januari hii?

Kuna wimbi la baadhi ya wachezaji wa United, hasa ambao hawapati nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kutaka kuondoka klabuni hapo. Iwe kwa mkopo au kuuzwa moja kwa moja, lakini wasiendelee kusugua benchi.

Jesse Lingard, Donny Van De Beek, Dean Henderson na Juan Mata ni miongoni mwa wachezaji wanausugua benchi muda mrefu. Baada ya kuona juhudi za Martial zimezaa matunda, nani atafuata nyayo?

Newcastle ni kama wameshakata tamaa na usajili wa Lingard kutokana na kushindwa kufikia makubaliano na United. Crystal Palace wanajitutumua kumsajili Van De Beek wakati huu ambao maongezi na United yanaendelea.

Spurs walionesha nia ya kutaka kumsajili Henderson wakati ule walipokua wakipambania kumbakizia Lloris, sasa wamefanikiwa na Lloris amebaki. Henderson ana nafasi yeyote Spurs? Kwa Mata, anahusishwa kurejea nyumbani – Hispania. Real Sociedad wanatajwa katika hili, watafanikiwa?


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe