Balotelli Alalama Kutoheshimiwa na Mashabiki wa Milan

Mshambuliaji wa Nice, Mario Ballotelli amelalamika kuwa mashabiki wa AC Milan wameshindwa kutambua mchango wake na kumheshimu baada ya kuitumikia klabu hiyo.

Nyota huyu alizungumzia tetesi za yeye kurejea kwenye klabu hapo, amesema kurejea kwa mara ya tatu klabuni hapo sio rahisi sana. Ana amini wapo mashabiki wengi tu wanao onesha moyo mgumu kwa yeye kurejea.

Kwenye ukurasa wake wa Instagramu, amelalamika kuwa wapo mashabiki ambao hawataki arejee klabuni hapo. Mashabiki hao wamekosa kumuheshimu na kutambua mchango wake klabuni pale.

Hata hivyo, anasisitiza kuwa bado hajutii nafasi yake na wakati alioutumia na klabu ya Milan, na kwa upande wake bado anawapenda mashabiki wa Milan.

2 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Habari nzuri

    Jibu

Acha ujumbe