Klabu ya Bayern Leverkusen chini ya kocha Xabi Alonso wanaendelea kukiwasha kunako ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga baada ya leo kushinda mchezo wao tena dhidi ya Fc Cologne.

Xabi Alonso na vijana wake wameendeleza rekodi yao ya ushindi msimu huu ambapo mpaka sasa wamekaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Ujermani wakiwa juu ya bingwa mtetezi kwa alama mbili.alonsoBayern Leverkusen mpaka sasa wamefanikiwa kucheza michezo saba katika ligi kuu ya Ujermani wakifanikiwa kushinda michezo sita kati ya saba, Huku wakidondosha alama moja tu dhidi ya klabu ya Bayern Munich.

Wapinzani wao wa karibu klabu ya Bayern Munich ambao ndio mabingwa watetezi wao pia wamefanikiwa kushinda mchezo wa leo kwa mabao matatu kwa bila dhidi ya Freiburg, Huku wakiendelea kua nyuma ya Bayern Leverkusen kwa alama mbili wakikamata nafasi ya tatu na alama zao 17.alonsoKocha Xabi Alonso tangu akabidhiwe klabu ya Bayern Leverkusen amefanikiwa kuibadlisha zaidi klabu hiyo na kua moja ya timu zinachocheza mpira mzuri, Lakini licha ya kucheza vizuri wanapata matokeo mazuri na mpaka sasa ndio vinara wa Bundesliga.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa