Bayern Munich Hawataki Kumuachia Davies Bure

Uongozi wa klabu ya Bayern Munich chini ya mkurugenzi wao Eberl amesema hawako tayari kumuachia bure beki wa kushoto klabuni hapo raia wa kimataifa wa Canada Alphonso Davies.

Mkurugenzi wa Bayern Munich Eberl akizungumza na waandishi wa habari alisema”Hakuna klabu ipo tayari kumpoteza mchezaji bure kwakua tu hawajafikia muafaka katika suala la kuongeza mkataba mpya, Kama mchezaji hataki kubaki hapa unatakiwa kufanya maamuzi”bayern munichBeki Alphonso Davies mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu ujao kwa maana mwezi Juni 2025, Lakini mpaka sasa inaelezwa hayupo tayari kuongeza mkataba mpya kwa wababe hao wa soka nchini Ujerumani.

Kauli ya mkurugenzi huyo wa Bayern Munich imelenga wazi kua watakua wako tayari kumuuza beki huyo mwishoni mwa msimu huu, Kwani wakiruhusu aendelee kukipiga klabuni hapo mpaka mwishoni mwa msimu ujao watampoteza mchezaji bure jambo ambalo hawako tayari.bayern munichBeki Alphonso Davies hajasaini mkataba mpya mpaka sasa ndani ya Bayern huku ikielezwa beki huyo ana mpango wa kujiunga na miamba ya soka kutoka nchini Hispania klabu ya Real Madrid na ndio sababu beki huyo amegoma kusaini mkataba mpya kwa mabingwa watetezi hao wa Ujerumani.

 

Acha ujumbe