Watano Bayern Munich Hatihati Kuikosa Arsenal

Kocha wa klabu ya Fc Bayern Munich Thomas Tuchel amesema wachezaji wake watano kwenye kikosi hicho kuelekea mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga.

Wachezaji kama Manuel Neuer, Kingsley Coman, Leroy Sane, Nous Mazraoui, pamoja na Aleks Pavlovic watakosekana kesho dhidi ya Heidenheim kwenye ligi kuu ya Ujerumani, Lakini pia watakua na hatihati ya kukipiga katika mchezo dhidi ya Arsenal.bayern munichWasiwasi mkubwa kwa klabu hiyo ni kua kati ya wachezaji watano ambao watakosekana katika mchezo wa kesho wachezaji wanne ni wachezaji wa kikosi cha kwanza wa klabu hiyo, Hivo ni wazi klabu hiyo itapata pengo kubwa kuwakosa wachezaji wake hao.

Hii inaweza kua taarifa nzuri kwa klabu ya Arsenal kuelekea mchezo wao wa hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya, Kwani kukosekana kwa wachezaji hao kunaweza kutoa faida ya kwa washika mitutu hao wa jiji la London.bayern munichKlabu ya Bayern Munich imekua kwenye wakati mgumu msimu huu kwani mpaka sasa wanaonekana wana nafasi kwenye taji moja tu ambalo ni ligi ya mabingwa ulaya, Kwani kwenye ligi kuu ya Ujerumani mpaka sasa wanaonekana kuutema ubingwa huo.

Acha ujumbe