Bayern Munich Yamfukuzia Ferlan Mendy

Miamba ya soka kutoka nchini Ujerumani klabu ya Bayern Munich inafukuzia saini ya beki wa kushoto wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Ufaransa Ferlan Mendy.

Bayern Munich wanaelezwa kufukuzia saini ya Ferlan Mendy kutokana na beki wao wa kushoto Alphonso Davies anatarajiwa kutimka klabuni hapo majira ya joto ambapo amegoma kusaini mkataba mpya.bayern munichKitu cha kufurahisha kutokana na taarifa hii ni kua Bayern wanamuhitaji Mendy kutoka Real Madrid, Huku taarifa kubwa kuhusu Davies ni kua atatimkia Real Madrid mwishoni mwa msimu, Hivo ni kama vilabu hivi viwili vinajaribu kuoneshana umwamba.

Beki Ferlan Mendy amekua na msimu bora sana akiw amoja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu ya Real Madrid mpaka sasa, Lakini kwakua Real Madrid imeonesha nia ya kumtaka Davies ina maana beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa atakua na wakati mgumu klabuni hapo.bayern munichWakati huohuo Ferlan Mendy anahusishwa na klabu ya Bayern Munich kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amemmwagia maua beki huyo kua ni bora zaidi duniani kwa nafasi yake, Huku ikielezwa amezungumza na uongozi wa klabu hiyo ili kumbakiza klabuni hapo.

Acha ujumbe