Bayern Munich Kumsajili Tah

Klabu ya Fc Bayern Munich ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa beki wa klabu ya Bayern Leverkusen raia wa kimataifa wa Ujerumani Jonathan Tah.

Bayern Munich wanataka kumsajili Jonathan Tah kwasababu wako kwenye mpango wa kumuuza beki wa kimataifa wa Uholanzi Mathijjs De Ligt ambaye kwasasa wanafanya mazungumzo na miamba ya soka kutoka nchini Uingereza klabu ya Manchester United.bayern munichBeki Jonathan Tah ameshaonesha taa ya kijani kua anataka kujiunga na wababe hao wa soka la Ujerumani, Hivo hali hii imewapa nguvu sana Bayern wakiamini wanaweza kunasa saini ya beki huyo ambaye amekua akifanya vizuri kwenye kikosi cha Bayern Leverkusen chini ya kocha Xabi Alonso.

Klabu ya Bayern Munich imeongeza hali ya kujiamini kua watapata saini ya beki Jonathan Tah kwakua beki huyo anataka kujiunga nao, Lakini pia wana uhakika wa kumuuza beki De Ligt jambo ambalo litawaongezea pesa ambayo itarahisishga kupata saini ya Tah ambapo mwanzoni ofa yao ilikataliwa na klabu ya Bayern Leverkusen.

Acha ujumbe