Bayern Munich Kumchukua Tah

Klabu ya Bayern Munich baada ya kukamilisha dili la kumuuza Mathijjs De Ligt kwenda klabu ya Manchester United sasa wamemgeukia beki wa klabu ya Bayern Leverkusen Jonathan Tah.

Vigogo hao wa soka kutoka nchini Ujerumani wamekua na mazungumzo na beki Jonathan Tah kwa kipindi cha miezi miwili sasa wakifanikiwa kukubaliana nae maslahi binafsi, Hivo kilichobaki ni kuhakikisha wanatoa ofa nzuri ambayo itakubaliwa na Bayern Leverkusen ili kukamilisha dili hilo.bayern munichBavarians wamemuachia beki De Ligt wakijua fika kua watafanya usajili wa beki mwingine wa kati na shabaha yao ni beki wa klabu ya Bayern Leverkusen Jonathan Tah raia wa kimataifa wa Ujerumani, Beki huyo ameonesha kila dalili anataka kucheza Bavarians msimu ujao kilichobaki ni Leverkusen kupewa kiasi ambacho wanakihitaji.

Beki Jonathan Tah amekua kwenye kiwango bora ndani ya kikosi cha Bayern Leverkusen chini ya kocha Xabi Alonso jambo ambalo limewavutia Bayern Munich kuhitaji huduma yake, Vyanzo mbalimbali kutoka nchini Ujerumani vinaeleza beki huyo kujiunga na Bayern ni suala la muda tu.

Acha ujumbe