Bayern Munich Wana Matumaini Makubwa ya Kumbakiza Musiala

Klabu ya Fc Bayern Munich wana matumaini makubwa ya kumbakiza kiungo mshambuliaji wao Jamal Musiala ambaye anakaribia kumaliza kandarasi yake ndani ya timu hiyo muda mchache ujao.

Mkurugenzi wa wa klabu ya Bayern Munich bwana Eberl wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumuongezea mkataba mpya Jamal Musiala alisema”Mkataba mpya kwa Musiala? Itakuwa vigumu lakini siyo jambo lisilowezekana.”

“Jamal anajua anachokipata akiwa Bayern. Hiki ndicho klabu iliyomfikisha kwenye kiwango cha juu.”

“Mazungumzo tayari yameanza na sasa yataimarishwa zaidi. Jamal anapaswa kuwa uso wa Bayern.”bayern munichKiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani mzaliwa wa Uingereza amekua moja ya wachezaji muhimu sana ndani ya klabu ya Bayern Munich, Hivo klabu hiyo haipo tayari kumuona anatimka ndani ya timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika na ndio maana jitihada za kumuongezea mkataba mpya ni kubwa kwelikweli.

Jamal Musiala inaelezwa anafukuziwa na vilabu kadhaa vikubwa barani ulaya ikiwemo klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza ambayo inamuona kama mbadala sahihi wa kiungo wao Kevin De Bruyne, Hivo Bayern Munich wana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha mchezaji huyo anabaki kwenye viunga vya Allianz Arena.

Acha ujumbe