Klabu ya Fc Bayern Munich wamepanga kuachana na mpango wa kutafuta mrithi wa Manuel Neuer ambaye ameumia mpaka siku ya mwisho ya usajili.

Klabu ya hiyo imekua kwenye mchakato wa kutafuta golikipa ambaye atakua mbadala wa golikipa wao namba moja Manuel Neuer ambaye amefanyiwa upasuaji, Hivo atakosekana kwa msimu mzima ambao umebakia. Bayern munichKlabu ya Bayern Munich imekua ikihusishwa na magolikipa kadhaa ikiwemo golikipa aliefanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia akiichezea timu ya taifa ya Croatia Dominik Livakovic, pamoja na Yann Sommer anayechzea klabu ya Borussia Monchebgladbach.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo amesema kua suala la golikipa ni jambo ambalo wanalifikiria na kulifanyia kazi, Lakini wako sokoni mpaka tarehe 31 Januari hii ambapo ndo itakua siku ya mwisho ya usajili hivo wataangalia watafanya maamuzi ya kusajili golikipa au wataachana na mpango huo.Bayern munichKlabu ya Bayern Munich kwa siku za karibuni imekua ikihusishwa sana na golikipa raia wa Uswisi Yann Sommer ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu na klabu ya Borussia Monchengladbach, Na klabu hiyo inaelezwa ipo makini zaidi na golikipa huyo ili kua mbadala wa muda wa Manuel Neuer.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa