Klabu ya Bayern Munich kutoka nchini Ujerumani wameripotiwa kutuma ofa ya pili kwa klabu ya Tottenham kwajili ya mshambuliaji wa klabu hiyo Harry Kane.
Bayern Munich walifanikiwa kutuma ofa ya kwanza kwa klabu ya Tottenham ambayo ilikua kiasi cha Euro milioni 70 ambayo ilikataliwa na sasa wametuma kiasi cha Euro milioni 80 ambayo wanaamini inaweza kuwashawisha Spurs.Mabingwa hao wa Ujerumani wanamuona Harry Kane kama mtu sahihi ambaye anaweza kuongoza safu yao ya ushambuliaji, Kwani tangu ameondoka Roberto Lewandowski hawajafanikiwa kupata mshambuliaji wa kiwango cha dunia.
Harry Kane amekua akiwindwa na vilabu tofauti tofauti barani ulaya katika dirisha hili la usajili ikiwemo Man United na Real Madrid, Lakini ni Bayern Munich pekee ambao wameonesha uthubutu wa kutuma ofa kwajili ya kuinasa saini ya mshambuliaji huyo.Taarifa zinaeleza kua mshambuliaji Harry Kane hana mpango wa kuondoka ndani ya ligi kuu ya Uingereza, Hivo Bayern Munich kama watafanikiwa kuishawishi klabu ya Tottenham kwa ofa ambayo wataweka mezani lakini watakua na kazi ya kumshawishi mshambuliaji huyo kutoka nje ya Uingereza.