Bayern Munich Kurudi kwa Palhinha Januari

Klabu ya Bayern Munich imepanga kurejea kwa kiungo wa kimataifa wa Ureno anayekipiga klabu ya Fulham Joao Palhinha mwezi Januari na kufanya jaribio la kumsajili kwa awamu nyingine.

Kiungo Joao Palhinha alihitajika na klabu ya Bayern Munich katika dirisha kubwa lililopita na dili kushindwa kufanikiwa katika siku za mwisho za dirisha hilo jambo ambalo inaonekana Bavarians hawakulikubali.bayern munichKiungo Joao Palhinha alikaribia kujiunga na mabingwa hao wa soka kutoka nchini Ujerumani lakini dili lake lilishindwa kufanikiwa kutokana na sababu tofauti tofauti ambazo hazikuweza kuwekwa wazi.

Mabingwa hao wa soka kutoka nchini Ujerumani wanaelezwa kuhitaji kujaribu kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno katika dirisha dogo la mwezi Januari kwani wanaamini atakua nyongeza nzuri ndani ya kikosi chao.bayern munichKiungo Joao Palhinha amekua mchezaji muhimu sana ndani ya klabu ya Fulham akionesha ubora mkubwa sana katika nafasi yake ya kiungo wa ulinzi, Ikiwa ni sababu iliyowavutia klabu ya Bayern Munich na kuhitaji saini yake.

 

Acha ujumbe