Bayern Munich Kuulamba Dili la Zirkzee

Klabu ya Fc Bayern Munich wanatajwa kupata asilimia 50% kwenye dili la mshambuliaji Joshua Zirkzee ambaye amejiunga na klabu ya Manchester United ya hivi karibuni.

Klabu ya Bayern Munich kuchukua asilimia 50% kwenye dili hilo kutoka kwa Bologna kutokana na kipengele  walichokieka kwenye mkataba wakati wanamuuza mchezaji huyo kwa klabu ya Bologna, Inaelezwa watachukua kiasi cha Euro milioni 21 kwakua dili hilo lina thamani ya Euro milioni 42.

Hii imekua kawaida kwa klabu kubwa kuweka kipengele cha kupokea kiasi cha pesa pale wanapumuuza mchezaji kwenye vilabu vingi vya daraja la kati, Jambo ambalo Bayern wamelifanya kwa usahihi mkubwa na sasa watakwenda kupokea

kamisheni yao kwenye dili hilo.bayern munichJoshua Zirkzee ambaye ndio mchezaji aliowaneemesha klabu ya Bayern Munich ameshafanikiwa kujiunga na klabu ya Manchester United, Huku leo ikielezwa amekamilisha vipimo vya afya klabuni hapo na kusaini mkataba wa miaka mitano ambao una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.

Acha ujumbe