Bayern Munich wameanza rasmi safari ya kutetea taji lao la Bundesliga kwa mtindo wa mabingwa, baada ya kuichapa Stuttgart kwa 5-1 katika mchezo uliowapa mashabiki wao sababu nyingine ya kuamini kuwa msimu huu unaweza kuwa wa kutawala tena. Kikosi cha Vincent Kompany kilionyesha ubora, utulivu na makali mbele ya lango, huku ushindi huo ukiwa wa pili mfululizo tangu msimu mpya uanze. Wiki iliyopita Bayern waliifunga Borussia Dortmund 2-1 na kutwaa German Super Cup, kabla ya kuendeleza kasi hiyo dhidi ya Stuttgart katika mchezo ambao uliishia kuwa onyesho la nguvu za mabingwa.

Bayern walifungua ukurasa wa mabao kupitia Dayot Upamecano, aliyefunga kwa kichwa kwa ustadi baada ya kupokea mpira wa kona uliopigwa na Joshua Kimmich. Stuttgart walikuwa na sababu ya kumshukuru kipa wao Fabian Bredlow, ambaye alifanya saves kadhaa muhimu kuwaweka ndani ya mchezo. Juhudi zake zilizaa matunda pale Josha Vagnoman alipousawazisha mchezo kwa shuti kali lililokwenda moja kwa moja kwenye nyavu. Lakini furaha ya Stuttgart haikudumu muda mrefu, kwani Bayern walirudi mbele baada ya Kimmich kutoa pasi nzuri na Michael Olise kuitumia nafasi hiyo kwa ustadi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Drama ikaendelea pale Vagnoman alipogeuka kutoka shujaa wa kusawazisha kuwa mchezaji aliyefunga kwenye lango lake mwenyewe. Aliteleza alipokuwa akijaribu kuondoa krosi ya Alphonso Davies, na mpira ukaingia kwenye nyavu na kuipa Bayern bao la tatu. Olise baadaye alidhani amefunga bao lake la pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Harry Kane, lakini VAR ikafuta bao hilo kwa sababu ya offside. Hata hivyo, Bayern hawakuacha kushambulia, na Aleksandar Pavlovic akaongeza la nne.
Saibari mwenyewe alikuwa sehemu ya habari kubwa ya mchezo huo. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, aliyesajiliwa kutoka PSV Eindhoven kwa takribani pauni milioni 43, alionyesha kwa nini Bayern walimwamini. Katika muda wa nyongeza, Saibari alipokea mpira na kwa akili akamlaza Luis Diaz katika nafasi nzuri, kabla ya mshambuliaji huyo kuongeza bao la tano na kukamilisha usiku wa goli nyingi kwa Bayern.

Ushindi huu unaongeza presha kwa wapinzani wao mapema kabisa katika msimu. Mabingwa hao tayari wameonyesha kuwa hawataki kupoteza muda, wakiwa na ushindi dhidi ya Dortmund na Stuttgart ndani ya michezo miwili.


