Borussia Dortmund (BVB) inaendelea kuwa klabu inayoteka soko la usajili kwa mara nyingine msimu huu. Baada ya Jadon Sancho, safari hii ni Erling Haaland.

Bado kuna hali ya sintofahamu kuhusu usajili wa Haaland msimu huu. Wakala wa mchezaji huyu – Mino Raiola ameshafanya vikao na baadhi ya vilabu kuhusu usajili wa mteja wake ambaye BVB wameweka wazi hawatomuuza kwa bei rahisi.

Endapo kunatimu yeyote itakayomuhitaji Haaland mwishoni mwa msimu huu, watapaswa kutoa dau la kuanzia pauni milioni 150 au zaidi. Japokuwa, mkataba wa mshambuliaji huyu unakipengele kitakachomruhusu kuondoka Dortmund kwa pauni milioni 75 ifikapo Juni,2022.

BVB, BVB Hawanapresha na Haaland Msimu Ujao., Meridianbet
Jadon Sancho na Erling Haaland

Kutokana na hali ya kiuchumi ilivyo kwa sasa na mambo mengine mengi, uongozi wa BVB haunashaka na usajili wa Haaland ambaye wanaamini atabaki klabu ni hapo kwa mwaka mmoja zaidi. Mkurugenzi wa Dortmund, Hans-Joachim Watzke amenukuliwa akisema “ninategemea Haaland ataendelea kuwa hapa msimu ujao.

“Sina shaka katika hilo. Mwaka jana hakuna mtu alituamini kuhusu Jadon Sancho mpaka siku ya mwisho na alibaki hapa mpaka sasa. Ninadhani (Barcelona na Real Madrid) wanautambua mkataba na msimamo wetu katika hili.”

Ukiachilia mbali suala la Haaland, Dortmund wapo tayari kumuachia Sancho kuondoka klabuni hapo endapo timu inayomtaka itatimiza vigezo walivyokubaliana na mchezaji huyo mwaka jana. Hadi sasa, Man United, Chelsea na Liverpool zinahusishwa na Sancho.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

BVB, BVB Hawanapresha na Haaland Msimu Ujao., Meridianbet

CHEZA HAPA

9 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa