Beki wa zamani wa klabu ya Ajax raia wa Uholanzi Daley Blind amekaribia kujiunga klabu ya Fc Bayern Munich baada ya kuelekea kufanya vipimo vya afya na klabu hiyo.
Beki huyo ambaye amevunja mkataba na klabu yake ya Ajax na kuondoka klabuni hapo baada ya kuitumikia kwa muda mrefu, Hivo mchezaji huyo anajiunga na mabingwa hao wa Ujerumani akiwa kama mchezaji huru.Beki huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye pia amewahi kuitumikia klabu ya Manchester United kwa misimu kadhaa, Anafanikiwa kujiunga na klabu ya Fc Bayern kwa mkataba wa miezi sita kama ambavyo taarifa zinaeleza yaani mpaka mwisho wa msimu huu.
Beki Daley Blind inaelezwa amekataa ofa mbalimbali za vilabu kutoka nchini Hispania na nchiini Ubelgiji ambazo zilionesha kuhitaji huduma ya beki huyo, Lakini beki huyo ameona klabu pekee ambayo anaweza kuitumikia kwasasa ni Bayern Munich.Beki Daley Blind anakwenda kujiunga na klabu ya Bayern Munich kwa mkataba wa miezi sita yaani mpaka mwisho wa msimu ndipo watakaa tena mezani kujadili hatma yake, Beki huyo amekua kwenye ubora kwa muda mrefu huku akifanikiwa kucheza vilabu bora na vikubwa barani ulaya.