Wakati wakiendelea kutafuta uhakika wa kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, Borussia Dortmund wameibuka kidedea kwenye fainali ya Kombe la Ligi, DFB Cup 2020/21.

BVB walitumia dakika 45 za kwanza kupachika magoli 3 yaliyowekwa kambani na Jadon Sancho (2) na Erling Haaland (1) kabla ya Haaland kuongeza la 4 katika kipindi cha pili. RB Leipzig wamejikuta wakiangukia pua kwa mara nyingine licha ya Olmo kuwapatia goli la kufuta machozi.

Dortmund, Dortmund Bingwa wa DFB Cup 2020/21., Meridianbet
Jadon Sancho akifurahia ushindi na Erling Haaland

Kocha wa Leipzig, Julian Nagelsmann ambaye anaondoka mwishoni mwa msimu huu na kujiunga na Bayern Munich, amekosa nafasi ya kubeba taji lake la kwanza akiwa na Leipzig. Badala yake, kocha wa Dortmund,Edin Terzic amekuwa kocha wa kwanza mwenye umri mdogo (miaka 38 na siku 195) kubeba kombe la DFB Cup tangu mwaka 1998/99 ambapo aliyekuwa kocha wa Weder Bremen, Thomas Schaaf (miaka 38 na siku 43) alipofanya hivyo.

Hili linakuwa ni kombe la 5 kwa Dortmund kubeba katika historia ya mashindano hayo.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Dortmund, Dortmund Bingwa wa DFB Cup 2020/21., Meridianbet

CHEZA HAPA

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa