Erling Haaland: Dortmund Wananilazimisha.

Wakati zikiwa zimesalia siku 14 dirisha dogo la usajili barani Ulaya kufungwa, Erling Haaland amefunguka kinachoendelea Borussia Dortmund.

Haaland anahusishwa na vilabu vikubwa barani Ulaya hii ni kutokana na uwepo wa kipengele cha kumsajili wa dau la £64M ifikapo Juni 2022. Real Madrid, Man United, Man City na Bayern Munich ni miongoni mwa vilabu vinavyohusishwa na mshambuliaji huyu.

Japokuwa Erling Haaland hakuwahi kusema chochote kwa kinachoendelea kuripotiwa kwenye vyombo vya habari, imefikia hatua ameamua kusema hali halisi. Baada ya kuisaidia BVB kushinda 5-1 dhidi ya Freigburg, Haaland amesema;

Miezi 6 iliyopita, nilichagua kutosema chochote kwa kuiheshimu klabu [Borussia Dortmund]. Lakini, sasa hivi klabu inanilazimisha kufanya maamuzi kuhusu hatma yangu muda huu. Hii inamaanisha kuwa, ninatakiwa kufanya maamuzi muda si mrefu.

Imeripotiwa kuwa, Dortmund wanataka kufanya kikao na Haaland pamoja na timu yake (wakala wake) ili kujua hatma yake ni nini. Je, anampango wa kuendelea kubaki BVB baada ya msimu huu au, anataka kuondoka klabuni hapo?


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe