Klabu ya Ujerumani inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo FC Schalke 04 imeondoa nembo ya kampuni ya Urusi inayohusika na uchimbaji na usambazajiwa wa gasi GAZPROM ambayo ndio mdhamini mkuu wa klabu hiyo kwenye jersey zake na sehemu zote kwenye klabu.

Kampuni ya GAZPROM, ambayo inamilikiwa na serikali ya Urusi, ilianza kuidhamini klabu ya FC Schalke 04 kuanzia mwaka 2007 kama mdhamini mkuu wa klabu hiyo, kutokana na tukio la nchi ya Urusi kuivamia Ukraine, klabu hiyo imesitisha ushirikiano kuanzia leo siku ya alhamisi.

FC Schalke 04

Kwenye waraka uliotolewa na klabu hiyo leo ulisomeka, “kufauatia maendeleo ya hivi karibuni, klabu ya FC Schalke 04 imeamua kuondoa nembo ya mdhamini mkuu GAZPROM kwenye jersey za klabu, na badala yake kutakuwepo na maandishi ya Schalke 04”

Pia chama cha soka barani ulaya  UEFA nacho kimelaani kitendo hicho na kuamua kuifuta nchi ya Urusi kuandaa mchezo wa fainali, ambao ulipangwa kufanyika jijini St. Petersburg, na kesho ijumaa watatoa tamko kuwa wapi fainali hiyo itachezwa.


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa