Beki wa kimataifa wa Croatia na klabu ya RB Leipzig Josko Gvardiol  amesema mpango wake ni kuendelea kukipiga kwenye klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani.

Beki Josko Gvardiol amekua ni mchezaji anaefatiliwa zaidi kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari, Huku vilabu mbalimbali vikubwa barani ulaya vikitajwa kuwania saini ya beki huyo wa kimataifa wa Croatia kutokana na ubora mkubwa mabao amekua akiuonesha.gvardiolBeki huyo anayekipiga RB Leipzig inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga amekua akionesha ubora mkubwa sana ndani ya klabu hiyo, Ni moja ya sababu inayofanya vilabu vikubwa barani ulaya kuhitaji saini ya beki huyo kwasasa.

Mkurugenzi wa klabu ya RB Leipzig alisema mchezaji huyo hauzwi na hawana mpango wa kumuuza kwasasa jambo ambalo beki huyo ameunga mkono kwa kusema mipango yake ni kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo kumalizia miezi yake sita iliyobakia.gvardiolJosko Gvardiol amefanya vilabu vingi kummezea mate kutoka na ubora ambao pia aliuonesha kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar mwaka jana akiwa na timu ya taifa ya Croatia. Vilabu vya Real Madrid, Liverpool, na PSG vinatajwa kuwinda saini ya beki huyo mdogo mwenye uwezo mkubwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa