Josko Gvardiol amesisitiza kuwa ana furaha katika klabu yake ya RB Leipzig lakini hataondoa uwezekano wa kuhamia Chelsea iwapo watamtaka huko Darajani.

 

Gvardiol Anafuraha Leipzig Lakini Azungumza Kuhusu Nia ya Chelsea

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa ni mada kubwa ya uvumi mwanzoni mwa msimu, huku Chelsea ikisemekana kuwa ofa ya pauni milioni 77 ikikataliwa na timu hiyo inayoshiriki Bundesliga.

Gvardiol baadaye alisaini mkataba mpya huko Leipzig na ameendelea kuvutia kutokana na kiwango chake anachokionyesha, lakini mazungumzo kuhusu uhamisho hayajaisha, na beki huyo wa kati alizungumzia uwezekano huo baada ya kuichezea Croatia dhidi ya Ubelgiji kwenye Kombe la Dunia.

Gvardiol amesema kwamba; “Unajua kilichotokea katika miezi michache iliyopita na kusema kweli sijui wakala wangu anashughulikia hili na tutaona kwani kwasasa nina furaha huko Leipzig.”

Gvardiol Anafuraha Leipzig Lakini Azungumza Kuhusu Nia ya Chelsea

Alipoulizwa maoni yake kuhusu Chelsea, mchezaji huyo alisema kuwa ni klabu kubwa nani anajua labda siku moja atakuwepo huko na inapendeza sana kuona kwamba mambo kama haya, hasa kwasababu kuna Mateo Kovacic hasa inabidi umuulize kama anamtaka.

Gvardiol alielezewa kama mchezaji ambaye ni bora zaidi Duniani na kocha wa Croatia Zlatko Dalic hapo jana, huku beki huyo akifurahia kiwango cha Kimataifa alichokionyesha katika Kombe la Dunia.

Gvardiol Anafuraha Leipzig Lakini Azungumza Kuhusu Nia ya Chelsea

Zlatko amesema kuwa kuwa bila shaka ni mchezaji mzuri anafanya kazi nzuri, kuwa hapa kweny tukio hili kubwa zaidi ni jambo kubwa kwake katika umri wa miaka 20 na ana furaha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa