Mshambuliaji wa Dortmund, Erling Haaland anatarajia kurejea mapema dimbani baada ya kupata taarifa njema juu ya jeraha lake.

Wasi wasi ulikuwa nyota huyu angekawia kurejea dimbani, na alitemwa kwenye kikosi kilichocheza Ligi ya Mabinwa dhidi ya Lazio, mechi ambayo walilazimisha sare ya bao 1-1.

Bosi Lucien Favre anaamini kuwa changamoto ya jeraha la Haaland ilikuwa ni kutokana na kucheza mechi nyingi, hivyo alihitaji kupata mda kidogo wa kupumzika.

Staa huyu amecheza jumla ya mechi 14 za Dortmund kwenye michuano yote msimu huu, akiwa ameanza kwenye mechi 13 kati ya mechi hizi na kucheka na nyavu mara 17.

Haaland: Nitarejea Mapema Tu!

Fomu yake imekuwa na ahadi njema katika mbio za Ligi na mchango wake kwenye Ligi ya Mabingwa. Kutokuwepo kwenye mechi ya Jumatano dhidi ya Lazio kulifanya staa huyu akose fursa ya kuongeza idadi ya magoli kwenye rekodi yake ya Ligi ya Mabingwa.

Mpaka sasa, staa huyu amefunga magoli 16 kwenye Ligi ya mabingwa, ambayo ni wastani wa goli moja katika kila dakika 56. Rekodi hii sasa itasubiri wakati staa huyu mwenye miaka 20 akitarajiwa kuwa atarejea dimbani mwezi januari.

Hata hivyo, staa huyu amechapisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa kuna taarifa njema kutoka kwa daktari wake, na anatarajia kuwa atarejea uwanjani mapema zaidi.


 

FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Haaland, Haaland: Nitarejea Mapema Tu!, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

20 MAONI

  1. Staa huyu amecheza jumla ya mechi 14 za Dortmund kwenye michuano yote msimu huu, akiwa ameanza kwenye mechi 13 kati ya mechi hizi na kucheka na nyavu mara 17

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa