Hertha Berlin Wamfuta Kazi Tayfun Korkut

Klabu ya Hertha Berlin wamesitisha mkataba na aliyekuwa kocha wao Tayfun Korkut kufuatiwa matokeo mabovu ya hivi karibuni na kupoteza kwenye mchezo wao dhidi ya Borussia Mönchengladbach.

Tayfun alichukua mikoba iliyoachwa na Pal Dardai mwishoni mwa mwezi Novemba, huku akianza vizuri kwa kukusanya pointi nne kwenye michezo miwili ya mwanzo, japo alipata kipigo kitatifu kutoka kwa Mainz, ila Hertha Berlin ilifurahia kufunga mwaka kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Borussia Dortmund kwenye mchezo wa mwisho mwaka 2021.

Hertha Berlin

Hertha Berlin haijafanikiwa kupata ushindi wowote kwa mwaka huu 2022, na wamepoteza michezo mitano mfurulizo, huku mchezo wa jumamosi ambao wamepoteza kwa 2-0 dhidi ya Mönchengladbach umewaweka kwenye nafasi ya pili kutoka mwisho.

Baada ya kumfuta kazi Tayfun, klabu ya Hertha Berlin wanamtafuta mrithi ambaye ataingoza timu hiyo kwenye michezo nane ya mwisho kwenye msimu huu.

“Baada ya tathimini na uchambuzi wa kina kwenye mfumo wa uchezaji, uongozi wa klabu ya Hertha Berlin umeamua kusitisha mkataba na Tayfun Korkut kwenye nafasi yake ya ukocha, na kuanzia sasa  hatakuwa sehemu ya klabu hii,”  waraka rasmi wa klabu ya Hertha ulisomeka.

“Tutoa taarifa kuhusu nani atachukua nafasi yake haraka iwezekanavyo tutakapo kamilisha maswala binafsi.”


SHAOLIN FORTUNES 100 LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

liverpool, Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe