Kane na Hat-trick ni Kama Pete na Kidole

Harry Kane alifunga hat-trick yake ya pili msimu huu wa Bundesliga wakati Bayern Munich ya wachezaji 10 ikiibuka na ushindi wa dakika 45 za pili na kuwashinda wachezaji tisa wa Darmstadt 8-0 kwenye uwanja wa Allianz.

 

Kane na Hat-trick ni Kama Pete na Kidole

Joshua Kimmich alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya dakika nne pekee, lakini kadi nyekundu za Klaus Gjasula na Matej Maglica zilihakikisha wenyeji wanapata faida wakati wa mapumziko, ikiwa ni mara ya kwanza kwa wachezaji watatu kutolewa katika kipindi cha kwanza cha mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Ujerumani.

Kane alifunga mabao matatu na kufikisha mabao 12 katika mechi tisa za msimu huu mpya wa Bundesliga.

Leroy Sane, ambaye alimtengezea Kane bao la tatu, alifunga mawili yake huku Thomas Muller pia akichangia kichapo kikali zaidi katika historia ya wageni.

Kane na Hat-trick ni Kama Pete na Kidole

Darmstadt walikuwa wamejizatiti dhidi ya mabingwa hao wa Bundesliga katika dakika 45 za kwanza za mchezo lakini bado ilikuwa ni ngumu kwa wao kupata chochote kitu wakiwa ugenini.

Muller alifunga bao lake la kwanza msimu huu kabla ya Musiala kumfunga Schuhen bao la saba kwa Bayern, na wakati kipa wa Darmstadt aliokoa mabao machache, akitamani asione timu yake ikipoteza kwa mabao mengi, hakuweza kumzuia Kane.

 

Acha ujumbe