Kocha wa Bayern Munich, Vincent Kompany amesema ataendelea kutathmini msimu wa timu hiyo baada ya fainali ya Kombe la Ujerumani wiki ijayo, lakini amesisitiza kuwa tayari wamejiwekea kiwango kikubwa kuelekea msimu ujao.
Bayern walihakikisha ubingwa wa Bundesliga mapema na sasa wana nafasi ya kutwaa mataji mawili ya ndani kwa mara ya kwanza ndani ya miaka sita. Aidha, walifika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kutolewa na PSG kwa jumla ya mabao 6-5.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Tutangoja kidogo kwa sababu bado tuna fainali muhimu ya Kombe la Ujerumani ambayo ina nafasi kubwa katika msimu wetu,” alisema Kompany kuelekea mchezo wa mwisho wa Bundesliga dhidi ya FC Köln.
“Kwa ujumla tumeshinda mechi nyingi, tumepitia hisia na uzoefu mkubwa, na wachezaji wengi wameendelea zaidi. Kiwango kimepanda na msimu ujao tunataka kuendelea kuimarika zaidi, hilo ndilo jukumu letu linalofuata,” aliongeza.
Kompany ameiongoza Bayern kutwaa mataji mawili mfululizo ya Bundesliga katika misimu yake miwili akiwa kocha mkuu. Timu hiyo pia imevunja rekodi ya mabao mengi ndani ya msimu mmoja wa Bundesliga baada ya kufunga mabao 117 huku ikiwa bado na mchezo mmoja mkononi. Rekodi ya awali ya mabao 101 ilikuwa imedumu tangu msimu wa 1971/72.
Bayern watacheza dhidi ya VfB Stuttgart katika fainali ya Kombe la Ujerumani itakayofanyika Berlin Mei 23, huku mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Max Eberl akisema bado hawajamaliza kazi yao msimu huu.
“Bado hatujamaliza. Tunaweza bado kushinda Kombe na kutwaa ‘double’. Hatukushinda Kombe kwa miaka sita lakini kile tulichokifanya hadi sasa, hasa kwenye ligi, ni kitu cha kipekee,” alisema Eberl.
Kompany pia alisema timu na mashabiki wana sababu kubwa ya kusherehekea mafanikio hayo, huku Bayern wakitarajia kufanya sherehe za ubingwa ndani na nje ya uwanja mwishoni mwa wiki hii mjini Munich. “Unaanza msimu ukiwa na matumaini ya kuinua tena taji la ligi na sasa muda huo umefika, hivyo tutaufurahia,” alisema Kompany.


