Ulimwengu wa soka la kisasa umegubikwa na mvutano wa nguvu kati ya klabu na mchezaji. Hili linaonekana kwa Robert Lewandowski msimu huu.

Ni dhahiri, Lewandowski hataki kuendelea kuitumikia Bayern Munich baada ya msimu huu. Anachokitaka ni kuondoka klabuni hapo kwenye majira haya ya usajili wa dirisha kubwa.

Suala lililopo hapa ni matakwa ya Bayern, klabu inasisitiza haitomuuza Robert licha ya kwamba mshambuliaji huyo amegoma kusaini mkataba mpya. Mkataba wake wa sasa unaisha mwishoni mwa msimu ujao na, Bayern wanaamini watambakiza klabuni hapo mpaka atakapomaliza mkataba wake.

Msimamo wa Bayern ni kinyume cha msimamo wa Lewandowski. Akiwa na timu yake ya Taifa kwa sasa, Robert amesema;

Muda wangu na Bayern umeisha. Sioni uwezekano wowote wa kuitumikia hii klabu. Bayern ni timu yenye msimamo na ninaamini hawatonibakiza, sitaki kuendelea kucheza kule tena. Usajili ni suluhisho sahihi. Nina imani hawatonizuia.

Bayern wanakazi ya kufanya katika hili. Tayari Corentin Tolisso ameshaachana na klabu hii kama mchezaji huru huku kukiwa na sintofahamu kuhusu Serge Gnabry ambaye naye, mazungumzo ya mkataba mpya hayanamuelekeo mzuri.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa