Marie-Louise Eta Aandika Historia Kwa Ushindi Wake wa Kwanza Bundesliga

Kocha wa muda wa Union Berlin, Marie-Louise Eta ameandika historia baada ya kupata ushindi wake wa kwanza tangu kuwa mwanamke wa kwanza kuinoa timu katika Bundesliga, kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mainz 05 Jumapili.

Marie-Louise Eta Aandika Historia Kwa Ushindi Wake wa Kwanza BundesligaEta aliteuliwa kuwa kocha wa muda mwezi Aprili baada ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Steffen Baumgart. Tangu uteuzi wake, kocha huyo amekuwa akipokea pongezi pamoja na baadhi ya maneno ya dharau kupitia mitandao ya kijamii kutokana na historia yake ya kuwa mwanamke wa kwanza kufundisha Bundesliga.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Baada ya kupoteza michezo miwili ya mwanzo akiwa kocha mkuu, Union Berlin ilipata sare dhidi ya Koln kabla ya hatimaye kupata ushindi huo muhimu dhidi ya Mainz. Eta alisema amefurahishwa sana na matokeo hayo baada ya juhudi kubwa walizoweka katika timu.

Marie-Louise Eta Aandika Historia Kwa Ushindi Wake wa Kwanza Bundesliga“Kikubwa kilikuwa kufanya kazi yetu vizuri, kupata pointi na kushinda michezo, na hicho ndicho tumekuwa tukikifanyia kazi kila siku,” alisema Eta katika mahojiano. “Kila wakati unataka kushinda mechi, na leo tumefanikiwa kufanya hivyo.”

Marie-Louise Eta Aandika Historia Kwa Ushindi Wake wa Kwanza Bundesliga

Kocha huyo pia alieleza kufurahishwa na namna timu yake ilivyocheza na kupambana hadi kupata ushindi huo muhimu ambao umeongeza morali kuelekea mchezo wa mwisho wa msimu. “Namna tulivyopata ushindi huu ilikuwa nzuri sana. Tumewekeza nguvu nyingi na ni jambo kubwa kupata pointi tatu pamoja na kuonyesha kiwango kizuri,” alisema.

Marie-Louise Eta Aandika Historia Kwa Ushindi Wake wa Kwanza Bundesliga

Union Berlin sasa itamaliza msimu wa Bundesliga kwa mchezo dhidi ya Augsburg Jumamosi, huku Eta akitarajiwa kurejea kuinoa timu ya wanawake ya klabu hiyo msimu ujao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.