Mino Raiola Atoa Maono Tetesi Za Usajili Wa Haaland

Wakala wa Mchezaji Erling Haaland, Mino Raiola anadai kwamba labda hakuwa makini sana kupelekea uhamisho wa Haaland kujiunga na Borussia Dortmund. Anahisi Mshambuliaji huyo anaweza kujiunga na timu yoyote anayeitaka.

Haaland amefanikiwa kujihakishia kuwa miongoni mwa washambuliaji bora duniani akiwa na umri wa miaka 20, huku klabu za Manchester City. Manchester United, Chelsea na Real Madrid wakionekana kutaka huduma ya mchezaji huyo majira yajayo ya joto.

Kocha wa United Ole alimfundisha Haaland katika klabu ya Molde ambapo alifanya vizuri, na alitaka kumsajili ajiunge na mashetani hao wekundu wa Manchester. Lakini Haalanda alijiunga na Borussia Dortmund ambapo amefanikiwa kufunga magoli 49 katika michezo 49 aliyocheza.

Maendeleo hayo ya Haaland yamemfanya Raiola kuwaza kuhusu Haaland kujiunga klabu yoyote duniani, kama angetaka alivyotoka klabu ya Salzburg.

Mino Raiola kuhusu Haaland
Mino Raiola Akiongea Na Wanahabari Kuhusu Haaland

“Na kuhusu Haaland, Kila mtu alikosea. Amefanya kazi kubwa sana kwa muda mfupi, tofauti na watu wengi walivyotegemea. Haaland yuko mbele ya ratiba yake na anaweza kujiunga na timu yoyote”, Alisema Raiola akiwa anaongea na chombo cha habari cha The Athletic.

Wakala huyo ambaye anafanya kazi na wachezaji wakubwa mbalimbali duniani kama Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba anaamini kwamba kwa sasa Haaland yupo tayari kujiunga na Klabu yoyote ile duniani.

Je, unahisi Haaland anafaa kujiunga na timu gani kwa kuzingatia moto wake wa sasa huko Bundesliga?


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

CHEZA HAPA

5 Komentara

    Vizuri

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Good

    Jibu

    Nc

    Jibu

    Haaland yupo hot kama cake

    Jibu

Acha ujumbe