Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani Thomas Muller amesema kuondoka kwa kiungo wa klabu hiyo Marcel Sabitzer aliyeelekea Manchester United ilikua taarifa ya kushtua kwao.
Mshambuliaji Muller amesema kuondoka kwa kiungo Marcel Sabitzer ndani ya klabu ya Fc Bayern Munich kuliwashangaza wachezaji wote ndani ya timu kwakua ilikua taarifa ya ghafla kwao, Lakini mshambuliaji huyo amesema amefurahi kwakua kiungo huyo ameelekea klabu ya Manchester United kwakua ni klabu kubwa duniani.Kiungo Marcel Sabitzer alifanikiwa kujiunga na klabu ya Manchester United katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili la mwezi Januari, Huku akielekea klabu hiyo ili kupata nafasi zaidi ya kucheza tofauti na klabu ya Bayern Munich ambapo amekua hapati nafasi ya kutosha.
Mshambuliaji Thomas Muller hakusita kumwaga sifa kwa kiungo huyo kwa kusema ni mtu mzuri na mchezaji mzuri pia, Lakini pia akisisitiza ana matumaini kibao kua mchezaji huyo ataweza kurejea kwenye dirisha kubwa na kuweza kuungana tena klabuni hapo.Kiungo Marcel Sabitzer amejiunga na klabu ya Manchester United kwa mkopo wa nusu msimu kuanzia Januari mpaka mwezi Mei msimu utakapokua umemalizika, Hivo mchezaji huyo anatarajiwa kurudi ndani ya klabu ya Bayern Munich katika dirisha kubwa la majira ya joto kwakua hakuna kipengele cha Man United kumnunua kwa mkataba wa kudumu.