Mshambuliaji mwenye umri mdogo kutoka nchini Ujerumani anayekipiga kwenye klabu ya Fc Byern Munich Jamal Musiala ameendelea kuweka rekodi kwa mabingwa hao watetezi nchini Ujerumani.

Jamal Musiala amefanikiwa kupiga pasi ya bao katika mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani dhidi ya klabu ya Schalke 04 ambapo klabu yake ilipata ushindi wa mabao mawili kwa bila.Huku kinda huyo akiongeza idadi ya mchango wa magoli klabuni hapo.musialaBaada ya kupiga pasi ya bao katika mchezo wa jana kinda huyo amefikisha pasi sita za mabao huku akiwa na mabao tisa na mchango wa magoli ukifika 15, Hii inatokana na uwezo mkubwa ambao amekua akiuonesha kijana huyo toka apewe nafasi klabuni hapo.

Baada ya mchezo wa jana dhidi ya Schalke 04 mchezaji huyo alifanikiwa kufikisha michezo 100 ndani ya klabu hiyo na kuweka rekodi kama kijana mwenye umri mdogo zaidi kufikisha michezo 100 klabuni hapo, Musiala anafikisha michezo 100 na klabu ya Fc Bayern akiwa na umri wa miaka 19 tu jambo ambalo halijawahi kufanywa na kinda yeyote.musialaPia mchezaji huyo ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kitakachoshiriki michuano ya kombe la dunia nchini Qatar mwezi ujao akiwa ni miongoni mwa vijana wadogo walioitwa wakiongozwa na Youssufa Moukoko anayekipiga Borussia Dortmund.

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa