Kocha wa klabu ya Bayern Munich Julian Nagelsmann ameingia matatani baada ya kumvaa mwamuzi aliyechezesha mchezo wao dhidi ya Borussia Monchengladbach jana.

Kocha Nagelsmann alionekana kufoka mbele ya mwamuzi baada ya mchezo wao dhidi ya Borussia Monchengladbach waliopoteza kwa mabao matatu jwa mawili, Kocha huyo alionekana kulalamikia kadi nyekundu ambayo alipewa beki wake Dayot Upamecano dakika ya nane tu ya mchezo.NAGELSMANShrikisho la soka nchini Ujerumani linaelezwa limemuandikia barua kocha huyo baada ya taarifa kueleza baada ya mchezo kumalizika alionekana kwenda kumfokea mwamuzi Tobias Welz, Hivo kocha huyo anatakiwa kutoa maelezo juu ya tukio hilo alilolifanya.

Kocha Nagelsmann wakati anazungumzo na wanahabari alieleza kua mchezaji wake Upamecano hakustahili kuoewa kadi nyekundu kwakua mgusano ulikua mdogo baina yake na mchezaji wa Borussia Monchengladbach, Lakini vilevile kocha huyo alikiri kua alivuka mipaka katika kukablilana na mwamuzi Tobias Welz.NAGELSMANKocha Nagelsmann yuko hatarini na kama ikitokea ikathibitika kua ana hatia baada ya kufoka mbele ya mwamuzi Tobias Welz, Basi koha huyo atakabiliwa na adhabu kali kwani shirikisho la soka nchini Ujerumani katika taarifa yake limeeleza kua linamchunguza kocha huyo kutokana na kauli zake ambazo sio za kiungwana na kiuanamichezo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa