Neuer na Ulreich Waongeza Mkataba Bayern

Magolikipa wawili wa klabu ya Fc Bayern Munich Manuel Neuer ambaye ni golikipa namba moja wa klabu hiyo pamoja na Sven Ulreich golikipa namba mbili wamefanikiwa kuongeza mikataba ndani ya Bayern.

Manuel Neuer ambaye pia ni nahodha wa klabu hiyo ambaye amerejea klabuni hapo siku za hivi karibuni ameongeza wa kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Ujerumani pamoja na Ulreich mpaka mwaka 2025.neuerGolikipa huyo namba moja wa klabu hiyo ambaye alijiunga na klabu hiyo mwaka 2011 akitokea Schalke 04 amekua na kiwango bora sana klabuni hapo tangu afike amekubali kusalia ndani ya viunga vya Allianz Arena kwa mwaka mwingine mmoja.

Sven Ulreich ambaye alikua anadaka zaidi wakati golikipa namba moja akiwa anauguza majeraha, Naye amekubali kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia Bavarians mpaka mwaka 2025.neuerManuel Neuer atakua ametimiza miaka 14 mpaka mwaka 2025 ambapo ndio utakua ukomo wa mkataba wake ambao ameusaini kwasasa, Ambapo itamfanya kua moja ya wachezaji waliofanikiwa zaidi klabuni hapo lakini pia waliodumu kwa muda mrefu.

Acha ujumbe