Mchezaji wa klabu ya Chelsea Calum Hudson Odoi ambaye kwasasa yupo kwa mkopo kwenye klabu ya Bayern Leverkusen ya nchini Ujerumani amesema kwasasa akili ipo nchini Ujerumani.

Winga Odoi ambaye anafanya vizuri ndani ya klabu ya soka ya Bayern Leverkusen inaelezwa kua klabu ya Chelsea ilihitaji kumrudhisha ndani ya klabu hiyo, Lakini Bayern Leverkusen waligomea mpango huo kwakua mkopo wa mchezaji huyo ulikua wa msimu mzuri.odoiKlabu ya soka ya Chelsea ambayo inapitia kiupindi kigumu ndani ya ligi kuu ya Uingereza pamoja na michuano mingine kwasasa, Ilifikiria kumrudisha mchezaji huyo ndani ya klabu hiyo baada ya timu hiyo kuandamwa na majeraha zaidi kwenye kikosi chake lakini ilishindikana.

Mchezaji Odoi amekua na wakati mzuri ndani ya Bayern Leverkusen amefunguka na kusema hana mazungumzo na klabu yake ya Chelsea kwasasa na kueleza akili yake ipo ndani ya klabu hiyo ya Ujerumani, Hii inaonesha mchezaji huyo wazi mchezaji huyo anafurahia maisha ndani ya klabu hiyo.odoiCalum Hudson Odoi atarejea ndani ya klabu ya Chelsea mwishoni mwa msimu huu pale ambapo mkopo wake ndani ya klabu ya Bayern Leverkusen utakapokua umemalizika, Lakini taarifa zinaeleza kua klabu ya Bayern Leverkusen ipo kwenye mchakato wa kumnunua mchezaji huyo jumla baada ya kuvutiwa na uwezo wa mchezaji.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa