Dani Olmo wa Hispania anasema hafikirii kuondoka RB Leipzig lakini “kila kitu kinawezekana”.
Chelsea, Manchester United na Real Madrid ni miongoni mwa klabu ambazo zimekuwa zikihusishwa na kutaka kumnunua Olmo wakati wa dirisha la usajili la Januari.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Hispania yuko chini ya mkataba na Leipzig, ambaye alijiunga nayo kutoka Dinamo Zagreb mnamo 2020, hadi mwisho wa msimu ujao.
Dani amesema hatarajii kuondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga anapojiandaa kurejea msimu huu baada ya kucheza Kombe la Dunia, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 pia hajakatazwa kuondoka.
“Nina kandarasi hadi 2024. Sifikirii kuhusu hilo kwa sasa, kuhusu mechi zinazofuata. Tuna mashindano matatu mbele yetu. Mambo yanatokea haraka sana katika soka, mambo yanaweza kubadilika kila wakati. Tulishinda DFB-Pokal msimu uliopita, na tunataka kufanya kila tuwezalo tena msimu huu ili kucheza kwa mataji tena.”
Olmo amesema ana mshauri wake ambaye anaishughulikia na anaangazia soka pekee. Amezungumza na Max Eberl ambaye ni mkurugenzi wa michezo Leipzig na mara chache, lakini hadi sasa hajazungumzia suala hilo.
Labda watazungumzia hilo tena hapa kwenye kambi ya mazoezi. Wataona kitakachotokea. Kila kitu kinawezekana.
Mchezaji huyo amefunga mabao matatu na kutoa asisti mbili katika mashindano yote ya Leipzig msimu huu.