Klabu ya Rb Leipzig imemtamani kiungo wa kimataifa wa Uholanzi Xavi Simons kwa uhamisho jumla kutokana na ubora ambao anauonesha kinda huyo ambaye yupo kwa mkopo klabuni akitokea klabuni hapo.
Mkurugenzi wa klabu ya Rb Leipzig Eberl anasema wataangalia namna ya kuweza kumbakiza Xavi Simons klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika mwaka 2024.Kiungo Xavi Simons amekua na kiwango bora sana ndani ya klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani, Huku akiwa amefanikiwa kuchangia mabao sita ndani ya klabu hiyo mpaka sasa akiwa amefunga matatu na kutoa pasi tatu za mabao.
Klabu ya Rb Leipzig wao wanaona kama wanaweza kuhakikisha wanaongeza muda wa kuendelea kummiliki mchezaji huyo kinda mwenye kipaji kikubwa raia wa kimataifa wa Uholanzi ambaye amewahi kukipiga timu ya vijana ya Barcelona.Klabu ya PSG wao kwa upande wao wanamtoa kwa mkopo mchezaji huyo ili kumpa ukomavu mkubwa, Kwani wana mipango mikubwa na mchezaji huyo siku za mbeleni kwakua wanaamini kwenye kipaji kikubwa alichonacho Xavi Simons.