Rb Leipzig Kumbakiza Xavi Simons

Klabu ya Rb Leipzig inaelekea kushinda mpambano wa kumbakiza kiungo wa kimataifa wa Uholanzi Xavi Simons ndani ya klabu hiyo licha ya ushindani mkubwa waliokutana nao.

Rb Leipzig wanamuhitaji Xavi Simons aendelee kuwatumikia kwa mkopo kama ambavyo aliwatumikia msimu uliomalizika, Kwani klabu yake ya PSG haipo tayari kumuuza hivo njia pekee ya kumpata kiungo huyo ni kuendelea kumtumia kwa njia ya mkopo kuelekea msimu ujao.xavi simonsKlabu hiyo imekutana na upinzani mkali sana katika kumuwania kiungo huyo kwani klabu ya Bayern Munich imekua ikipambana kwa kiasi kikubwa kumpata kiungo huyo, Lakini kiungo Xavi Simons inaelezwa ameonesha taa ya kijani kwa klabu ya Leipzig kua yupo tayari kuwatumikia.

Klabu ya Manchester United inaelezwa pia ilikua inafukuzia saini ya Xavi Simons huku wao wakielezwa walikua wanahitaji kumnunua kabisa na sio kumchukua kwa mkopo, Lakini mpaka sasa Rb Leipzig ndio wanaonekana kukaribia kushinda mpambano huu mkali uliohusisha vilabu vitatu.

Acha ujumbe