Klabu ya Real Madrid unaweza ukasema kazi imebaki kwao tu kwa beki raia wa kimataifa wa Canada anayekipiga kwa mabingwa wa Ujerumani klabu ya Bayern Munich Alphonso Davies.
Unaweza kusema kazi imebaki kwa Real Madrid kwani inafahamika kua beki Alphonsi Davies hana mpango wa kusaini mkataba mpya ndani ya viunga vya Allianz Arena, Hivo vinara hao wa soka nchini Hispania wanapaswa kumaliza kazi kwa kutuma ofa yao kwa Bayern Munich.Mkurugenzi wa klabu ya Bayern Munich Eberl aliweka wazi kua itawabidi kufanya maamuzi kama mchezaji huyo hataki kusaini mkataba mpya, Huku maamuzi wanayotarajia kuyachukua ni kumuuza mchezaji huyo kuliko aondoke bure.
Taarifa zinaeleza kua Real Madrid wanaandaa ofa rasmi kwajili ya kuituma kwa klabu ya Bayern Munich, Kwajili ya kuweza kupata saini ya beki Alphonso Davies ambaye ameonesha wazi hataki kusaini kandarasi mpya klabuni hapo.Beki Alphonso Davies amekua na kiwango bora sana dnani ya klabu ya Bayern Munich tangu apate nafasi mara ya kwanza, Huku akigeuka mchezaji muhimu kabisa klabuni hapo lakini ameonesha wazi anataka changamoto mpya baada ya kugoma kuongeza mkataba klabuni hapo.